KESI YA LEMA KUJULIKANA LEO



Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, leo, anatarajia kujua hatima ya dhamana ya kesi ya uchochezi inayomkabili.

Lema anashikiliwa katika mahabusu ya Magereza ya Kisongo mjini Arusha.

Wakili wake, Peter Kibatala amesema walikata rufaa chini ya hati ya dharura kuomba Mahakama isikilize kesi hiyo mapema.

Amesema waliamua kufuata maelekezo ya Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Mosha ya kuwataka kukata rufaa.

Katibu wa mbunge huyo, Innocent Kisanyage amesema rufaa hiyo itasikilizwa leo saa tatu asubuhi baada ya kukamilisha mambo yanayotakiwa.

Lema alirudishwa mahabusu kutokana na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kukataa kupokea ombi lake la kufanya marejeo ya uamuzi wa kunyimwa dhamana.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mosha alisema uamuzi uliofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi umeegemea kifungu cha Sheria cha Makosa ya Jinai CPA 148, hivyo kilimtaka mshtakiwa kukata rufaa siyo kuomba Mahakama hiyo kufanye rejea,

Rufaa hiyo itasikilizwa na Jaji Fatuma Massengi, huku Lema akitimiza siku ya 26 tangu apelekwe Gereza la Kisongo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.