ZAIDI YA MILIONI 24 TASLIMU ZAPATIKANA KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA LA SHULE YA SEKONDARI MWADUI
Jana katika KANISA LA KIINJILI LAKILUTHERI TANZANIA usharika wa Ebeneezer kanisa kuu
Shinyanga kulifanyika harambee kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala wa shule ya sekondari Mwadui inayomilikwa na
KKKT dayosisi kusini mashariki ya ziwa Victoria, ambapo zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 24 taslimu, nje na ahadi zilipatikana.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi makamu mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee hiyo ndugu Anderson Lyimo alisema “ Shule ya sekondari ya Mwadui ilianzishwa mnamo mwaka 1976 ikiwa chini ya mgodi wa WILLIAMSON DIAMONDS LTD na mwaka 1996 mgodi huu ulijitoa na shule hii ikawa chini ya KKKT usharika wa Mwadui.”
“Kwa
sasa shule hiyo imekuwa ni moja ya shule zinazofanya vizuri katika ufaulishaji
wa wanafunzi kwenda kidato cha tano. Pia shule hii imeanzisha masomo ya kidato
cha tano na sita kwa michepuo ya PCM, PCB, CBG, HKL na HGK”
Akieleza baadhi ya changamoto nyingi zinazoikumba shule hiyo ni pamoja na ukosefu wa jengo la utawala hivyo kumuomba mgeni rasmi kusimamia harambee hiyo.
Akieleza baadhi ya changamoto nyingi zinazoikumba shule hiyo ni pamoja na ukosefu wa jengo la utawala hivyo kumuomba mgeni rasmi kusimamia harambee hiyo.
“Tunakamuomba mgeni rasmi uweze kuendesha harambee hii ili tuweze kupata fedha za kutosha kwa ajili ya kuanza ujenzi
wa jengo la utawala wa shule yetu”
Akizungumza
katika harambee hiyo mgeni rasmi ndugu ASA MWAIPOPO, amewapongeza sana wadau na
watu wote waliojitokeza katika harambee hiyo
kwani ni sehemu mojawapo ya kumtumikia Mungu.
“Hii kazi mliyokuja kuifanya, ni kwa
ajili ya elimu ya watoto wetu kwa maisha yao ya baadae. Biblia inasema mkamate sana elimu usimuache aende zake,
mshike maana yeye ni uzima wako”(mithali 4:13).
Naye
askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania, dayosisi kusini mashariki
ya ziwa Victoria, Dr. Emmanuel Joseph Makala katika mahubiri yake aliwasihi
wakristo kutokukataa wito walioitiwa.
“Wito wa Mungu kwa mwanadamu ulianzia
katika bustani ya Edeni baada ya Adamu kutenda dhambi na akajificha, pamoja na
dhambi alizotenda, bado Mungu alimuita
naye akaitikia'' alisema askofu.
“Pamoja na kwamba dhambi inasononesha, inahuzunisha na kuaibisha bado Mungu hata leo anakuita.”
“Pamoja na kwamba dhambi inasononesha, inahuzunisha na kuaibisha bado Mungu hata leo anakuita.”
“Yawezakuwa wito akuitiao Mungu ni juu
ya utoaji sadaka, hivyo utakapotoa sadaka yako, hilo litakuwa itikio la wito wa
sauti ya Mungu, nayo sadaka yako itakuwa manukato mbele za Mungu na utabarikiwa
zaidi”
Askofu Dr. Emmanuel Joseph Makala, Askofu wa KKKT - DAYOSISI KUSINI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA akitoa neno wakati wa ibada.
Mtunza hazina wa Usharika wa Ebeneezer Gladness Sikawa akisoma matangazo wakati wa ibada
MC wa harambee hiyo ndugu Albert Kasa toka Mwanza akitoa maelekezo juu ya harambee hiyo
Makamu mwenyeiti wa kamati ya maandalizi ya harembee ndugu Anderson Lyimo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi
Mchungaji msaidizi wa Dean kanisa kuu Ebeneezer Shinyanga, Jackson Maganga (kulia) akiwa na Mkuu wa jimbo la Shinyanga mjini mchungaji Gacha, wote wawili wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi
Mkuu wa shule ya Sekondari Mwadui, Mchungaji Yohana Nzelu (kushoto) akiwa na mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya harambee
Katibu mkuu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria mchungaji Daniel Mono (kulia), makamu mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Anderson Lyimo (katikati) pamoja na ndg Albert Kasa wakiwa ibadani.
Askofu Dr. Emmanuel Makala akikabidhi kiasi flani cha mchango wake kwa MC
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya harambee, mzee Gabriel Shoo akijiweka sawa kwa ajili ya harambee hiyo
Mtunza hazina wa usharika Gladness Sikawa, pamoja na baadhi ya washarika wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi
Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya harambee wakitoa michango yao.
Mary Dafa, mjumbe wa kamati ya maandalizi
Edna Shoo, mjumbe mojawapo wa kamati ya maandalizi.
Mchungaji Ordorous Gunda, mkuu wa jimbo la Maswa
Askofu Dr. Emmanuel Makala akimkabidhi mgeni rasmi cheti cha heshima ya kuitikia wito wa kushiriki shughuli hii.
Baadhi ya washarika wakiwa ibadani
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi