WOMEN FORCE WAKABIDHI JENGO LA CHOO MAALUM CHA WASICHANA SHULE YA MAPINDUZI B SHINYANGA


Mwenyekiti wa Kikundi cha Women Force , Rebeca Mapolu akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kikundi cha wanawake maarufu ‘Women Force’ kimekabidhi jengo la choo maalum cha wasichana lenye thamani ya shilingi 3,918,000/= kwa Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga.

Hafla fupi ya makabidhiano ya Jengo maalum la wasichana kwa ajili ya kujistiri na kubadilisha taulo kwa watoto wa kike imefanyika leo Ijumaa Machi 7,2025 shuleni hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mwenyekiti wa Kikundi cha Women Force bi. Rebeca Mapolu amesema wamejenga na kukabidhi jengo hilo la wasichana ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka 2025 lakini pia kama sehemu ya utamaduni wao wa kusaidia jamii kama yalivyo malengo ya kikundi chao.
“Tumekuwa tukitoa michango yetu katika shida na raha mfano Mei 20220 tulitoa msaada wa vifaa kinga dhidi ya Uviko – 19 katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga, Machi 2021 tulitembelea wafungwa wanawake katika Gereza la Shinyanga na kutoa msaada wa mahitaji maalum, Novemba 2023 tulitoa viti vitano vya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na leo Machi 7, tumeweka alama hapa katika shule ya Msingi Mapinduzi B kwa kujenga jengo dogo la choo maalum cha wasichana chenye thamani ya shilingi 3,918,000/=”,ameeleza Rebeca.

“Kwa kuzingatia kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka 2025 yenye kauli mbiu ‘Wanawake na wasichana : Tuimarishe haki, usawa na uwezeshaji. Sisi kama wanawake tunaojiamini katika kusaidia na kuhamasisha jamii katika kukuza usawa, haki na uwezeshaji wa wanawake na wasichana kuweza kujiamini na kupata haki na usawa katika uwezeshaji ndiyo maana Wanachama wa Women Force kwa pamoja tuliona umuhimu wa kuwathamini wasichana wadogo wa shule hii ya msingi ili waweze kupata haki na usawa katika kujiamini na kuendelea kupata elimu ili kufikia ndoto zao”,ameongeza Rebeca.
Muonekano sehemu ya jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B

Aidha Rebeca amefafanua kuwa Kikundi cha Women Force kimeanzishwa mwaka 2020 kikiwa na wanachama 15 na sasa kina wanachama 19 kikiwa na malengo ya kusaidiana kwenye shida na raha, kuinuana kiuchumi ndani ya chama, kusaidia jamii inayowazunguka na kufurahi kwa pamoja.

Amesema licha ya mafanikio pia wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokuwa na kitega uchumi wa kikundi ambapo kikundi kipo kwenye mchakato wa kutafuta mradi utakaowezesha kuongeza kipato kwa mwanachama mmoja mmoja na kikundi kwa ujumla badala ya sasa wanachangishana fedha kama walivyofanya na kufanikisha ujenzi wa chumba maalum cha wasichana katika shule hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro amekipongeza Kikundi cha Women Force kwa mshikamano walionao na namna wanavyosaidia kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

“Women Force mmefanya kazi nzuri. Maisha hayana maana kama hatutatui changamoto za wengine. Women Force mmejikita kutatua changamoto katika shule hii, tunawapongeza sana kwa ujenzi mliofanya. Mlichofanya ni kikubwa sana,” ameeleza Mtatiro.
Mhe. Mtatiro amesema ni muhimu kwa wadau wengine kuungana na serikali katika kutatua changamoto zinazokabili jamii, akisisitiza umuhimu wa kuongeza matundu ya vyoo katika shule.

"Naagiza Uongozi na Kamati ya shule iitisheni kikao na wazazi mkubaliane kiwango cha kuchangia ili ujenzi wa vyoo uanze”,amesema Mtatiro.

“Women Force wameonesha mfano mzuri, wameleta athari chanya katika jamii nasi Serikali tutaendelea kuwapa ushirikiano. jengo ni zuri limejengwa kwa viwango bora kwa gharama nafuu. Naomba patunzwe vizuri pawe ni kwa ajili ya watoto wetu wa kike”,amesema Mtatiro.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mapinduzi B, Japhet Tibesigwa Jasson, amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,145, ambapo wavulana ni 552 na wasichana ni 593.

Hata hivyo, amesema kuwa shule hiyo ina matundu ya vyoo sita pekee, ambapo wasichana wanatumia matundu manne na wavulana matundu mawili akisisitiza kuwa shule inahitaji matundu 50 ya vyoo ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi wote.

TAZAMA PICHA
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro (katikati) akiongoza uzinduzi wa jengo la choo maalum cha wasichana chenye thamani ya shilingi 3,918,000/= kwa Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro (katikati) akiongoza uzinduzi wa jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro (kulia) akifungua koki ya maji katika jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Sehemu ya ndani sehemu ya jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Sehemu ya ndani sehemu ya jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro (katikati) akizungumza nje ya jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Muonekano sehemu ya jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Mwenyekiti wa Kikundi cha Women Force , Rebeca Mapolu akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Mwenyekiti wa Kikundi cha Women Force , Rebeca Mapulu akimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ngokolo, James Msimbang'ombe akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mapinduzi B, Japhet Tibesigwa Jasson akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la choo maalum cha wasichana katika Shule ya Msingi Mapinduzi B, iliyopo katika kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga lililojengwa na Kikundi cha Women Force
Muonekano wa vyoo katika Shule ya Msingi Mapinduzi yenye jumla ya wanafunzi 1,145, ambapo wavulana ni 552 na wasichana ni 593.
Shule hiyo ina matundu ya vyoo sita pekee, ambapo wasichana wanatumia matundu manne (kushoto) na wavulana matundu mawili (kulia). Shule hii inahitaji matundu 50 ya vyoo ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi wote.

Post a Comment

Previous Post Next Post