Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Anamringi Macha amewataka wananchi wa mkoa huo kutunza amani ya Nchi yetu ya Tanzania.
Hayo ameyasema leo katika ibada ya Jumatano ya majivu iliyofanyika katika kanisa la KKKT usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga
“Lakini niseme moja ya jambo linguine kubwa ni kuiombea hii nchi, tunaposema tuimbee hii nchi inawezekana ikawa ni mazoea. Lakini kwa bahati nzuri hata majumbani kwetu tuna vyombo vya habari, tunazo televisheni, tunazo redio na hata hizi simu zetu tunazo tukiangalia, nafikiri tunaweza tukajitazama sisi tukajiringanisha na nchi zinazotuzunguka
Tunapojifikiria sisi tujiombee ,tuiombee nchi yetu tujaribu kungalia kule Congo kaskazini ni kitu gani kinachofanyika na kama ni kweli tunaangalia katika vyombo vya habari ni vita viko watu hawana Amani lakini tukienda kule Sudani watu wanauana ni mapigano yanayoua mamia kwa mamia. tukienda kule masharika ya kati kule waizrael na watu wa Gaza ukiangalia ni shida kubwa hakuna Amani, tukienda kule urusi na Ukrain tunakuta nako ni shida namaeneo mengine mengi sana. Hivi sisi ni nani maana hapa tunakuwa kama kakisima, tena tuliombee taifa letu wakati huu wa Kwaresma na nyakati zingine zijazo”
“Namshukuru sana Baba mchungaji amegusia habari ya uchaguzi katika nchi yetu. Uchaguzi husababisha vita kama tusipokuwa na mkono wa Mungu akaunyoosha na sisi tukatenda yale yanayostahili. Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na kwa hiyo kila mmoja wetu awe na wajibu wa kutekeleza kile kinachostahili ,lakini tumuombe Mungu atuongoze katika kuweza kupata viongozi watakaoweza kutuongoza vema katika ngazi za udiwani, ubunge na hata Rais.”
“Tuzidi kumuombea Rais wetu, Dr samia Suluhu Hassan. Kwa kweli lazima tukiri naye Mungu amempa ujasiri, amempa naeema, amempa nguvu na upeo pamoja na hekima za kuweza kuliongoza Taifa letu. Hadi sasa hivi tunaendelea na ustawi. Tunaweza tukasema kwamba tunayo mapungufu lakini mapungufu haya NI changamoto na ni sehemu ya misha lakini jitihada zipo za kuhakikisha nchi yetu iwe na ustawi” Alisema Anamringi Macha.