MUKWALA AONDOKA NA HATRICK MECHI DHIDI YA COASTAL UNION





 

TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.


Imekuwa siku nzuri kwa mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Steven Dese Mukwala aliyefunga mabao yote matatu ya Wekundu wa Msimbazi leo, dakika za 30, 45’+2 na 56.


Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 22, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nne na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.


Kwa upande wao Coastal Union baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao 24 za mechi 22 sasa nafasi ya tisa katika ligi ya timu 16.

Post a Comment

Previous Post Next Post