LEAH ULAYA AREJESHEWA URAIS WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA


Na Isaac Masengwa - Masengwa Blog

Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania ulioketi kati ya Desemba 15 - 16, 2022 jijini Dodoma katika ukumbi wa JAKAYA KIKWETE CONVETION CENTER umemrejeshea Leah Ulaya nafasi yake ya Urais wa Chama hicho baada ya kusimamishwa na baraza la chama hicho tangu tarehe 16 Septemba 2021.

Rais huyo alisimamishwa nafasi hiyo na baraza la chama hicho kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kutengeneza mazingira ya kutofanyika uchaguzi wa kujaza nafasi ya katibu mkuu wa chama hicho baada ya aliyekuwepo kufariki dunia

Pia sababu nyingine ni kwamba kulikuwa na taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali, ambapo baada ya ukaguzi walipelekewa taarifa katika vikao vyao huku kurasa zilizomtaja na kumtaka Leah awajibike hazikuonekana hivyo baraza hilo kuamua kumsimamisha kusubiri mkutano mkuu wa Chama 2022 ambao ulisubiriwa kuamua ama aendelee kuwa Rais wa Chama au aondelewe kabisa.

Baada wajumbe kufikia agenda hiyo Bi. Leah Ulaya alipewa nafasi ya kujitetea mbele ya mkutano mkuu dhidi ya tuhuma hizo. Katika majibu yake, Bi Leah alieleza kuwa hizo hazikuwa za kweli bali ilikuwa nia ovu iliyotengenezwa na aliyekuwa katibu Mkuu wa chama hicho Ndg. Deus Seif ili kumchafua Rais wa chama hicho na kuonekana kuwa kulikuwa na msuguano mkubwa ndani ya uongozi wa CWT Taifa uliopelekea kukiyumbisha chama. Aliongeza kuwa nia ya Rais huyo ilikuwa ni kufuata katiba na kanuni za chama

Baada ya utetezi huo Bi Leah alipisha kikao hicho ili wajumbe wa mkutano mkuu wajadili na kuamua hatma ya kiongozi huyo mkubwa wa chama hicho.

Wajumbe wa Mkutano huo kwa pamoja waliridhishwa na majibu ya utetezi wa Bi. Leah Ulaya na kubaini kuwa hizo zilikuwa hila tu ndani ya uongozi wake na kwa sauti moja waliamua kumrejeshea nafasi yake kubwa ya uongozi ndani ya chama hic

Akiongea baada ya kurejeshewa nafasi hiyo Rais wa Chama hicho Bi. Leah Ulaya amesema kuwa baada ya haya kutokea alinyamaza kimya wala hakufunua kinywa chake kwa kipindi chote tangu aliposimamishwa nafasi hiyo bali alimwachia Mungu mwenyewe aamue.

Pia amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa kuiona haki iko wapi na kufanya maamuzi hayo kwa maslahi mapana ya chama hicho.

Katika hatua nyingine Mkutano mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania umemthibitisha Japhet Maganga kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu baada ya aliyekuwa Katibu mkuu wa Chama hicho Deus Seif kufukuzwa uanachama na chama hicho kupitia mkutano mkuu huo.

Deus Seif amefukuzwa uanachama wa CWT baada ya kukutwa na hatia na mahakama ya Tanzania Kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka na matumizi mabaya ya fedha za chama hicho iliyompelekea tarehe 28 Juni 2022 yeye pamoja na wenzake akiwemo aliyekuwa Mtunza hazina wa Chama hicho Ndg Abubakary kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.

Post a Comment

Previous Post Next Post