KATIBU MKUU KKKT DKMZV ATAMBULISHA TAREHE YA KUMSIMIKA ASKOFU MTEULE DKT. NZELU

Katibu Mkuu wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Bi. Happiness Geffi ametangaza kuwa Mei 14, 2023 ni tarehe rasmi ya kusimikwa kwa Askofu mteule Mch. Dkt. Yohana Ernest Nzelu aliyechaguliwa na mkutano mkuu wa Dayosisi hiyo ulioketi Desemba 9, 2022

Katibu Mkuu amesema hayo wakati wa ibada ya Jumapili ya Desemba 11, 2022 katika usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga wakati akiwatambulisha wageni kutoka nchini Marekani.

Pia amewashukuru washarika kwa kuombea mkutano mkuu huo na Mungu ameonekana.

" Nitumie nafasi hii kuwashukuru washarika wote wa dayosisi yetu kwa maombi yenu ya kuombea mkutano mkuu uliofanyika juzi, umekuwa mkutano mkuu mzuri kuliko mikutano yote iliyowahi kufanyika katika dayosisi hii" Alisema Katibu mkuu.

Post a Comment

Previous Post Next Post