Helena Mashaka (13), mwanafunzi wa darasa la saba shule ya Shahende
iliyopo Kata ya Butobela, mkoani Geita, amechomwa mikono yake kwa moto
na Mama yake kwa tuhuma za kuiba shilingi 30,000 na kupelekea mwanafunzi
huyo kushindwa kufanya mitihani yake ya kuhitimu.
Akizungumza
kwa njia ya simu, Mtendaji wa Kijiji hicho Edgar Michael, amesema
alipata taarifa ya mtoto huyo kujeruhiwa kutoka kwa mwalimu mkuu wa
shule hiyo majira ya saa 2:00 asubuhi akidai kuwa kuna binti amechomwa
moto na Mama yake na ameshindwa kufanya mitihani.
Baada ya
kupata taarifa hiyo wakamfuatilia mzazi kisha wakamkamata na kudai
alifanya tukio hilo kwa sababu mtoto huyo aliiba shilingi 30,000
Mpaka
sasa mzazi huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo kidogo cha
Polisi kilichopo Kata ya Bukoli, na mwanafunzi amepelekwa Zahanati ya
Bukoli kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Aidha Mtendaji huyo
amesema taratibu zinaendelea ili mwanafunzi huyo aweze kupata nafasi ya
kurudia kufanya mitihani hiyo ya kuhitimu kwa mwaka 2023.
Chanzo - EATV NEWS