KOCHA ALIYEAZIMWA NA SIMBA AZUA BALAA HUKO MALAWI

MPANGO wa Simba kumtumia kocha Juma Mgunda katika mechi ya mkondo wa kwanza ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Nyasa Big Bullets ya Malawi siku ya Jumamosi hii umekwama.

Simba ilimuazima Mgunda kutoka Coastal Union baada ya kocha Zoran Maki kutimka klabuni kwa kupata dili nono Al Ittihad ya Misri.

Hata hivyo haitamtumia tena baada ya kubaini hana cheti cha Leseni A ya CAF, licha ya ukweli ameisomea kozi ya daraja hilo.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ni kwamba mabosi wa Simba wamwamua kumpeleka Kocha wa timu ya Wanawake, Simba Queens, Sebastian Nkoma ili kuokoa jahazi.

Awali iliaminika vyeti vya Mgunda vipo TFF na ilikuwa rahisi kwao kuvituma CAF, lakini imebainika havijatoka.

Mgunda tayari alishaondoka na kikosi jana Alhamisi asubuhi na kuanza kuinoa ikiwa Malawi ikijiandaa na mchezo dhidi ya Nyasa utakaopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa wa Bingu jijini Lilongwe.

Mmoja wa viongozi wa Simba (jina limehifadhiwa) alithibitisha Nkoma ataondoka nchini leo Ijumaa asubuhi ili kuinusuru Simba isikutane na rungu la CAF kama itakosa kuwa na kocha mwenyewe vigezo kusimamia mechi za michuano ya CAF.

Post a Comment

Previous Post Next Post