Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi kuu Tanzania katika kikao chake cha Agosti 26, 2022 ilipitia mwenendo wa matukio mbalimbali kwenye ligi na kufanya maamuzi
Yanga imetozwa kiasi cha Tsh. 1,000,000/= baada ya mashabiki wake kurusha chupa uwanjani katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania uliopigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Katika mchezo dhidi ya Coastal Union Yanga imetozwa faini ya Tsh 500,000/= kwa kosa la kufanya mabadiliko kwa mikupuo minne badala ya mikupuo mitatu kama inavyoelekezwa kwenye kanuni.
Mwamuzi aliyechezesha mchezo huo Raphael Ikambi ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa raundi tatu baada ya kushindwa kutafsiri sheria
Ni katika tukio la kiuongo wa Coastal Union Mtenje Albano kumfanyia rafu mbaya mlinzi wa Yanga Yannick Bangala
Kamati imewakumbusha wachezaji wote na maafisa wa benchi la ufundi kuzingatia mchezo wa kiungwana Fair Play
Tags:
michezo