Mtendaji Mkuu wa klabu ya Asante Kotoko, Nana Yaw Amponsah ameshukuru kwa zawadi alizopewa na Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu.
Kabla ya mchezo wa jana wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya miamba hiyo ya Ghana, Mwenyekiti Mangungu alimkabidhi jezi , vikombe na majani ya chai ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano.
Baada ya zawadi hizo, Nana ameushukuru Uongozi huku akituombea dua kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja michuano ya ndani.
Nana ameongeza kuwa anaamini tuna kikosi imara chenye uzoefu ambacho kinaweza kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.
“Naushukuru uongozi wa Simba kwa zawadi hii naamini itaendelea ushirikiano na mshikamano baina yetu,” amesema Nana.
Mchezo huo wa kirafiki ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa magoli 4-2
Tags:
michezo