HII NDIO HALI HALISI ALIYONAYO MOLOKO PAMOJA NA KUTAKA KUTOLEWA KWA MKOPO


Kabla ya msimu huu kuanza telesis zilikuwa nyingi kumhusu winga Jesus Moloko kuwa pengine angetolewa kwa mkopo

Hata hivyo dakika 45 za mchezo wa ngao ya Jamii dhidi ya Simba zilitosha kuwakumbusha wananchi yule Moloko aliyesajiliwa msimu uliopita

Moloko ni kama amepindua meza akiwa tayari ameyoa pasi moja ya bao lililofungwa na Bernard Morrison katika mchezo wa ligi Kuu dhidi ya Coastal Union ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-0

Katika mchezo huo Moloko alipata majeraha na kuwapa hofu wananchi pengine angekaa nje kwa muda mrefu

Habari njema ni kuwa Moloko amerejea uwanjani akiendelea na maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Azam FC ambao utapigwa Septemba 06, 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Ni huyu huyu Moloko ndie aliyewaliza Azam FC msimu uliopita akifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 2-0 kwa Yanga.

Alipiga bao la kideoni ambalo kabla ya Yanga walipiga pasi takriban 22. Septemba 06 Azam wanaye tena

Post a Comment

Previous Post Next Post