WAZAZI WAWAOGESHA WATOTO DAWA ZA MVUTO WA MAPENZI ILI WAOLEWE - SHINYANGA




Picha haihusiani na habari yetu Baadhi ya wazazi katika kata ya Ilola , wilayani Shinyanga wamedaiwa kuwaogesha watotobwao wa kike dawa za mvuto wa mapenzi ili wapate wanaume wa kuwaoa na kujipatia utajiri wa mifugo.

Mratibu wa miradi kutoka shirika la Rafiki - Sido mkoani humo Mariamu Maduhu amebainisha kuwa baadhi ya wazazi katika eneo hilo huwaogesha kwa dawa ijulikanayo kama samba ili wapate wanaume, huku wakiachishwa masomo na wengine kuambukizwa maradhi.

"Tumekumbana na mwanafunzi ambaye aliogeshwa 'samba' akaolewa na kuacha masomo. Lakini hakudumu kwenye ndoa yake akaachika huku tayari akiwa ameshaambukizwa virusi vya Ukimwi" alisema Maduhu.

Naye mkuu wa idaracya maendeleo ya jamii wilayani Shinyanga, Deus Mhoja amesema jamii bado inapaswa kuendelea kupewa elimu juu ya ukatili hasa kwa watoto ambao ndio waathirika wakubwa na hata kuzima ndoto zao

Post a Comment

Previous Post Next Post