MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA WAUNGANA PAMOJA, WASEMA USHABIKI SIO UADUI

Baadhi ya mashabiki wa klabu ya Simba na yanga mkoani Kagera, wameungana na kuwa kitu kimoja baada ya kuanzisha kikundi chao kiitwacho Bukoba Simba na Yanga (BSY).

Mashabiki hao wameamua kufanya hivo wakijua kuwa ushabiki sio uadui na kwenda mbali zaidi kwa kuamua kuanzisha kikundi hicho kilichoanza na watu 70 na mpaka sasa kikundi hicho kina wanachama zaidi ya 300.

Mmoja wa wanachama hao alisema kuwa moja huo utakuwa muhimu sana kwani wamekuwa na utaratibu wa kusaidiana katika shida na raha bila kujali huyu anatoka timu ipi.

Lakini pia imewajengea umoja hata pale timu moja inaposhinda wanapongezana

Post a Comment

Previous Post Next Post