Sherehe ya harusi huko Tunisia ilikwama baada ya mamake bwana harusi kuamuru mwanawe amtupe bi harusi aliyetambulika kama Lamia Al-Labawi kwa sababu alikuwa 'mfupi na 'mwenye sura mbaya.' Mamake bwana harusi alisema bi harusi alikuwa na sura mbaya. Picha: Mirror.co.uk. Chanzo: UGC Mirror.co.uk iliripoti kuwa mamake bwana harusi alikutana na bibi harusi kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa harusi, baada ya kuona tu picha zake kabla ya siku hiyo.

Baada ya kumuona Lamia ana kwa ana, mama wa bwana harusi alikata tamaa. Jina la bwana harusi halijawekwa wazi vile vile tarehe ya harusi hiyo haikutajwa kwenye vyombo vya habari nchini humo.
Lamia aliyevunjika moyo alienda kwenye blogu yake kuomboleza kuhusu tukio hilo, akisema kwamba alishangazwa na kitendo cha mamake mchumba wake wakati huo. Alisema maandalizi ya harusi yalimgharimu sana. Tukio hilo lilizua mjadala na hisia kutoka kwa watu mitandaoni; @official_nat8 alisema: "Wasichana wafupi kama sisi tunahitaji haki. Huu ni mchezo. Dada, usilie juu ya hili. Mungu akuepushie tu na risasi mbaya unayotaka kuoa mvulana wa mama."
@skincarealadunni alisema: "Mwache msichana ajiondoe kwa sasa maana hii tayari ni ishara mama mkwe atakuwa akichunguza ndoa yao." @princessbunmid alisema: "Urembo wasemavyo, huwa machoni pa anayependa tu…… huyu dada ni mrembo ila sio machoni pa kaka huyu." Wakati huo huo, Legit.ng hapo awali iliripoti kwamba bibi harusi aliachwa mataani siku ya harusi yake wakati jamaa ambaye alikuwa amechumbiana naye kwa miaka 10. Sasha Aristide, 29, alikuwa ametumia miaka mitatu kupanga harusi na mpenzi wa maisha yake bila kujua tukio la kufedhehesha lililokuwa likimsubiri siku hiyo.
Mwanamke huyo ambaye ni muuguzi alisema alikutana na Kevin Hyppolite, meneja wa ofisi, miaka 10 iliyopita na akampenda, mambo yalikuwas shwari wakichumbiana. Mnamo Desemba 2017, wapenzi hao wawili walikuwa wamechumbiana na kuanza kupanga harusi ya kifahari ambayo ingegharimu KSh 2.1 milioni (N7.6m).
Tags:
habari