KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUTUNZA NYARAKA ZA MIRADI YA SERIKALI

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Sahil Geraruma

Na Kareny Masasy - Shinyanga

KIONGOZI wa mbio za mwenge 2022 kitaifa Sahil Geraruma amewataka wataalamu wote wa halmashauri na taasisi zote za serikali nchini zinazotekeleza miradi inayozinduliwa na kuwekwa jiwe la msingi zisimamamie vyema utunzaji wa nyaraka .

Kiongozo Sahili amesema hayo leo Ijumaa Julai 29, 2022 wakati akizindua vyumba viwili vya madarasa ya shule ya Sekondari Mwakata na shule ya sekondari Mwalimu Nyerere zilizopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.


" Nipende kutumia nafasi hii kuzitaka halmashauri na taasisi zote za serikali nchini, zinapotekeleza miradi ya serikali ni lazima kusimamia vyema utunzaji wa nyaraka za miradi hiyo ili kuweza kuweka kumbukumbu za mradi na kusaidia kufuatilia uhalisia wa gharama za mradi" alisema Sahil.

Sahili ameongeza kuwa makosa yaliyojitokeza kwenye miradi hiyo wayarekebishe ili kuifanya miradi hiyo kukamilika kwa ufanisi zaidi.

"Kasoro nilizoziona kwenye ujenzi wa vyumba hivyo na kukamilika nikutoweka kipaumbele eneo analokaa mwalimu darasani yaani kiti na meza, kutokujipanga vizuri katika miradi ili iende vizuri kwani mtu anayesimamia akipata dharura anayeachiwa awe makini kusimamia na kutekeleza"alisema Geraruma.

Naye mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga amesema kuwa halmashauri hiyo imefanikiwa kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi sita yenye thamani ya sh Millioni 874.6

Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Mwakata yenye wanafunzi 254 imekamilisha vyumba viwili vya madarasa ambavyo vimegharimu kiasi Cha sh millioni 40 huku mapato ya halmashauri ni Tsh millioni 13,serikali kuu Millioni 27 na michango ya wananchi Tsh milioni 4.

Pia mkuu wa shule ya sekondari ya Mwalimu nyerere Mwalimu Nyerere mwalimu Kafuru Songoro amesema kuwa ujenzi wa vyumba vya madarasa vitatu imegharimu kiasi Cha sh Millioni 60 ambapo ambapo mpaka sasa zimetumika kiasi Cha sh Millioni 51.

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Sahil Geraruma akikagua madarasa ya shule
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Sahil Geraruma akikagua madarasa ya shule
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Sahil Geraruma akikagua madarasa ya shule

Post a Comment

Previous Post Next Post