
Kiungo wa Yanga Salum Abubakar SureBoy akiwa katika majukumu yake
KIUNGO wa klabu ya Yanga Salum Abubakar SureBoy leo akatengeneza historia ya kipekee kwa wachezaji wa kitanzania baada ya klabu yake ya Yanga kuibuka na ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar katika pambano la mwisho la Ligi Kuu ya NBC linalopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo majira ya saa kumi kamili jioni ambapo klabu ya yanga imeibuka na ushindi wa goli moja kwa bila
Mchezaji huyo ambaye kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee wa kitanzania kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu bila kupoteza mchezo hata mmoja akiwa na klabu mbili tofauti ya Azam na Yanga.
Mwaka 2014 Azam FC walitwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara bila kufungwa ambapo na leo yanga amefanikiwa kutwaa ubingwa akiwa na Yanga bila kufungwa