MPINA AMVAA WAZIRI BASHE NJE YA BUNGE, ADAI KUWA WAZIRI ALILIDANGANYA BUNGE

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina

MBUNGE wa jimbo la Kisesa nchini Tanzania, Luaga Mpina amesema Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alilidanganya bunge kwa kutoa takwimu mbili tofaui kwenye jambo moja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mpina ameeleza hay oleo Alhamisi tarehe 30 Juni, 2022, akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa bunge muda mchache baada ya Spika kumnyima kuomba utaratibu kwa suala ambalo limepitwa na wakati.

Hata hivyo Mpina alitumia fursa hiyo na waandishi wa habario kueleza kile ambacho alitaka kuomba utaratibu kuhusu mtu kusema uongo bungeni.

Mbunge huyo ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa machachari bungeni amesema tarehe 18 Mei, na 24 Juni 2022 bashe amekuwa akimtuhumu kuwa anapotosha.

“Nilimtaka Spika atoe ufafanuzi anayepotosha Bunge ni Mpina au Bashe kwasababu wakati anawasilisha bajeti yake aya ya 264 alieleza mwenendo wa bei za mbolea na baadae kwenye kuhitimisha pia akataja mwenendo wa bei kwa takwimu tofauti na zile za awali.

“Takwimu zake za asubuhi zilikuwa zinatofautiana na zile za jioni kwa mfano kwenye mbolea ya DAP zinatofautiana kwa dola 64, bei ya UREA inatofautiana kwa dola 491 sasa hizi tofauti hizi ndiyo nikauliza uhalali wa hizi takwimu anazotumia Waziri ni zipi na bunge lifuate takwimu gani,” amehoji Mpina na kuongeza;

“Amekuja tena baadae ameeleza FOB rate na CIF rate ambayo kwenye hotuba yake para ya 264 mtu anaweza kwenda kusoma kama hayo maneno yametumika.”

Amesema “takwimu ukizikosea huwezi kuzirekebisha kwa kujisafisha kwa maneno tu kutamka unatakiwa uende uone between the line uone mahala panapozungumziwa.”

Amesema Waziri katika hotuba yake amezungumzia tu bei za mbolea mwenendo katika soko la dunia amekuja tena huku wakati anahitimisha akasema anakuja nataarifa za benki ya dunia lakini zinatofautiana.

Amesema katika hitimisho lake alishindwa kuanisha hizo bei za asubuhi zilikuwa za aina gani na hizo za jioni ni zipi “kwa sababu ni jukumu la anayetoa takwimu kueleza anamaanishha nini sio wasikilizaji wanaokusikliliza na si watumiaji wa takwimu ambao wanapaswa kuata zikiwa hazina mkanganyiko.”

Amesema wakati anatoa hoja yake ya mbolea alieleza kuwa bei za mbolea zinazotolewa na Serikali kutokuwa na uhalisia wa soko.

“Nikasema suala la mboela kupanda hazijasababishwa na vita ya Urusi na Uviko-19 peke yake, kuna kupanda kwingine ambapo tunasabbabisha sisi wenyewe.”

“Tulifika mahala ambapo mfumo wetu wa ununuzi wa pamoja tulikuwa tunafanya pre qualification lakini pia tulikuwa tunafanya due diligence tunaenda mpaka kwenye viwanda duniani kukagua viwanda na kupatana bei na hapa ndani ya nchi tulikuwa na bei elekezi kabla ya huu mfumo tulikuwa na bei za zaidi ya laki moja na baada ya kuingiza mfumo bei zikashuka hadi 40,000 bila ruzuku yeyote.”

Alisema baadae Serikali ilifuta mfumo huo wa manunuzi ya pamoja na bei elekezi “na matokeo yake wafanyabioashara wamepandisha bei na kudanganya wanapofika hapa nchini na wale wanaouzia wananchi wanapandisha “matokeo yake mfuko wa mbolea leo Urea inauzwa 130,000. Mimi naamini bei hizi tumezifikia kutokana na kukosekana na usimamizi wa mbolea nchini,”

“Na niliweka wazi hata Waziri mwenyewe kuna maeneo amelalamika juu ya watu kuongeza bei za mbolea na mpaka akawakamata watu waliouzia wakulima kwa bei kubwa.

“Hakuna mahala popote nilipopotosha kuhusu takwimu zangu zipo clear na nilitumia hotuba ya wizara ya kilimo mwanzo mwisho hakuna takwimu zilizotengenezwa na Mpina pale wao ndio wamejichanganya wamekuja na takwimu mbili tofauti na hawakufafanua mbele ya umma,” amesema.

Post a Comment

Previous Post Next Post