JAMAA AWADANGANYA WANAKIJIJI WAKABOMOA MISIKITI, ATOKOMEA KUSIKOJULIKANA NA MABATI

Mwanaume wa Nigeria anadaiwa kudanganya vijiji kadhaa kubomoa misikiti yao, akiwaambia ‘’NGO yake ya kigeni’’ ingejenga majengo mapya makubwa, mamlaka katika jimbo la kaskazini la Jigawa zilisema.

Lakini alitoweka baada ya kukusanya paa, madirisha na milango ambayo iliondolewa kwenye misikiti ‘’midogo’’.

Mshukiwa huyo ambaye polisi wamemtaja kama Abba Haruna, 21, anadaiwa kuuza vifaa hivyo.

Msemaji wa mahakama katika jimbo la Jigawa, Abbas Rufa’i Wangara, aliambia BBC kuwa misikiti 14 iliathirika.

Usaini Wanzam Ilyasu, mtawala wa kimila katika kijiji kimoja ambaye pia alizungumza na BBC, alisema mshukiwa huyo hata alilipa vibarua waliobomoa msikiti wao wa jumuiya.

Alisema mtu huyo aliwataka waundaji wa vitalu vya ujenzi wa eneo hilo kuanza kusambaza vifaa kwenye eneo linalodaiwa kuwa la ujenzi.

Lakini mtuhumiwa huyo alipoondoka, hakurudi tena.

Alikamatwa baada ya maafisa wa msikiti katika jamii nyingine aliyoitembelea kutilia shaka na kuzusha tahadhari.

Ingawa mshukiwa alishtakiwa kwa mara ya kwanza wiki jana, habari za tukio hilo lisilo la kawaida zinaendelea kusambaa.

Mshukiwa bado hajasema lolote na anatarajiwa kurejea katika mahakama ya hakimu mjini Kiyawa siku ya Alhamisi.

Post a Comment

Previous Post Next Post