SIMBA SC NA YOUNG AFRICANS SC KUPAMBANA LEO KWENYE NGAO YA JAMII KUIKARIBISHA LIGI KUU YA TANZANIA BARA !!!
Anaandika Mzee wa Atikali
Septemba 25, 2021
1. Usuli
Watani wa Jadi Nchini, SIMBA SPORTS CLUB na YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB, watamenyana leo kwenye uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa "Estadio de Lupaso" saa 11 jioni kugombea Ngao ya Jamii kuashiria kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu 2021/2022.
Manazi wa YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB @ "YANGA" ,@ "KUALA LUMPUR" ,@ "DAR ES SALAAM YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB" , @ "TIMU YA WANANCHI", iliyoanzishwa mwaka 1935, wamekuwa wakijinasibu kuwa, kihistoria, timu yao ndio wafalme kwenye Ligi ya kabumbu nchini. Nao manazi wa SIMBA SPORTS CLUB, iliyoanzishwa 1936 ikitoka ubavuni mwa "YANGA" na kujiita "QUEENS FC", "EAGLES", "SUNDERLAND" kabla ya kubadili jina mwaka 1971 na kujiita SIMBA SPORTS CLUB @ "WEKUNDU WA MSIMBAZI", @ "MNYAMA" , wamekuwa wakijimwambafy kuwa, kihistoria, wao ndio wafalme wa Ligi nchini.
Nikiwa kama "Mzee wa Atikali", nimefanya utafiti wa kina kwa kuyatabarazi magazeti mbalimbali kama vile "Tanganyika Standard" (lililoanzishwa Januari 1, 1930), "Ngurumo" (lililoanzishwa April 15, 1959), " Uhuru" (lililoanzishwa Desemba 9,1961), "Nationalist" ( lililoanzishwa April 17, 1964), "Daily News"( lililoanzishwa April 26, 1972) na mengine mengi yanayochapishwa sasa hapa nchini ambayo kwayo nimepata takwimu lukuki. Aidha, nimefukunyua makavazi mbalimbali kwavile teknolojia ya utunzaji wa kumbukumbu, kama iliyopo sasa, haikuwepo zamani.
Matokeo ya Utafiti huu mujarab yanaainishwa bayana kwenye "Atikali" hii ambayo inalenga kumaliza ubishi uliopo kati ya manazi wa timu hizi mbili.
2. Mtanange wa Kwanza wa Ligi
Ligi ya kabumbu Tanzania Bara ilianzishwa mwaka 1965 ambapo mtanange wa kwanza wa Ligi kati ya watani, SIMBA na "YANGA", ulipigwa Juni 7, 1965. "YANGA" iliifunga SIMBA bao 1-0 lililofungwa katika dakika ya 15 na mshambuliaji mahiri wa timu hiyo enzi hizo, Mawazo Shomvi, baada ya kuwapiga chenga mabeki wote wa SIMBA na kuweka mpira "nyavu ndogo".
Hivyo, "YANGA" ndio waasisi wa ushindi mechi za Ligi za watani wa jadi.
3. Bingwa wa Kwanza wa Ligi
SIMBA Ilishinda ubingwa wa kwanza wa Ligi ilipoanzishwa mwaka huo wa 1965. Hivyo, SIMBA ndio waasisi wa Ubingwa wa Ligi ya kabumbu nchini.
4. Idadi ya Mechi "YANGA" ilizoshinda
Toka mwaka 1965 hadi leo, "YANGA" imeshinda mechi 38 kati ya mechi 106 za watani kwenye Ligi.
5. Idadi ya Mechi SIMBA ilizoshinda
SIMBA imeshinda mechi 31 kati ya mechi hizo 106.
Hivyo, 38-31=7. Hii inamaanisha "YANGA" imeshinda mechi 7 zaidi. Kwavile timu hizi hukutana mara mbili tu katika Ligi Kuu kwa mwaka, itaichukua SIMBA takriban miaka 4 kuifikia rekodi hii iwapo itashinda mechi zote 7.
6. Idadi ya Sare za Watani wa Jadi
Katika Mitanange hiyo 106, sare za watani wa jadi ni 37.
7. Idadi ya Magoli ya kufunga ya "YANGA"
"YANGA" imetupia kambani kwa SIMBA mara 151.
8. Idadi ya Magoli ya kufunga ya SIMBA
SIMBA imecheka na nyavu" za "YANGA" mara 136.
Hivyo, 151 - 136 = 15. Hii inamaanisha "YANGA" imefunga magoli 15 zaidi ya SIMBA.
9. Idadi ya Magoli ya Kufungwa "YANGA"
Toka 1965, "YANGA" imefungwa na SIMBA magoli 136 kwenye Ligi.
10. Idadi ya Magoli ya Kufungwa SIMBA
SIMBA imefungwa na "YANGA" magoli 151.
Hivyo, 151 - 136 = 15. Hii inamaanisha SIMBA imefungwa na "YANGA" magoli 15 zaidi.
11. "Cleen Sheets"
Toka mwaka 1965 hadi leo, "YANGA" ina "Cleen sheets" 44 wakati SIMBA inazo 32 tu.
Hivyo, 44- 32 = 12. Hii inamaanisha "YANGA" ina "Cleen sheets" nyingi zaidi.
12. Idadi ya Mataji ya Ligi
Toka Ligi ianzishwe mwaka 1965, "YANGA" imenyakua ubingwa wa Ligi ya kabumbu nchini mara 27 wakati SIMBA imenyakua mara 22.
Hivyo, 27 - 22 = 5 ikimaanisha "YANGA" imeizidi SIMBA kwa mataji 5. Ili SIMBA iweze kuifikia rekodi ya "YANGA", inabidi iwe inautwaa ubingwa huu mfululizo hadi mwaka 2026!.
13."YANGA" ndiyo timu ya kwanza kuutetea ubingwa wao wa Ligi mara nyingi zaidi (1968, 1969, 1970, 1971 & 1972).
14. "YANGA" ndio waasisi wa "Vipigo vya Mbwa mwizi" kwenye mechi za watani ambapo Juni 1, 1968 "YANGA" iliikung'uta SIMBA 5-0.
15. SIMBA ndiyo inashikilia rekodi ya kutoa "Kipigo kikubwa cha Mbwa mwizi" kwenye mechi za watani ilipoifunga "YANGA" mabao 6-0 Julai 19, 1977.
16. SIMBA imetoa mfungaji pekee wa "Hat trick" kwenye mechi za watani, ABDALLAH KIBADENI "KING", ambaye alifunga katika dakika ya 10, 42 na 89 hapo Julai 19, 1977.
17. SIMBA ndio waasisi wa "Kuweka mpira Kwapani" kwani Machi 3, 1969 SIMBA iligoma kuingiza timu uwanjani kwakuwa "YANGA" ya mwaka huo ilikuwa bora maradufu kuliko ile ya 1968 iliyowafunga 5-0 hivyo ikaogopa kupokea kichapo kikubwa zaidi! Gazeti la "Ngurumo" la Machi 4, 1969 likaandika "Sunderland Yaikimbia Yanga". FAT ikaipa "YANGA" ushindi wa pointi 2 na magoli 2.
18. "YANGA" imetoa mchezaji ( KITWANA MANARA "POPAT" (183 ) anaeshikilia rekodi ya kuweka mpira kambani mara nyingi zaidi toka Ligi ianzishwe mwaka 1965. KITWANA ni baba yake mkubwa HAJI MANARA. MOHAMED HUSSEIN "MMACHINGA" (151) na JOHN BOCCO "ADEBAYOR" wanamfuatia kwa mbali sana.
HAJI MANARA, pia, aliwahi kudadavua kuhusu ukweli huu Mei 17, 2018-
"Waandishi mkachunguze mtabaini baba yangu mkubwa, Kitwana, ndiye mfungaji bora wa muda wote. Yule alikuwa hatoki uwanjani bila goli na ukizubaa anakupiga nyingi. Kitwana alikuwa balaa nyie ooh...
19. "YANGA" imetoa mchezaji ( KITWANA MANARA ) aliyekuwa na uwezo wa kufunga magoli ya vichwa kuliko mchezaji mwingine yeyote. Mengi ya magoli yake ya kichwa aliyafunga kutokana na kona za ABRAHAMAN JUMA ( Nahodha wa "YANGA", Mzizima United na Taifa Stars). Wajihi wa KITWANA (jitu la miraba minne lililopanda hewani) ulipelekea ishindikane kuruka nae hewani! ADAM SABU, MARTIN KIKWA na ABEID MZIBA ni "Cha Mtoto" kwa KITWANA MANARA!.
20. "YANGA" imetoa mchezaji wa kwanza TZ Bara kucheza "Professional Football" ( KITWANA). KITWANA alienda kucheza mpira wa kulipwa Kenya 1963.
KITWANA MANARA alikuwa na talanta ya kipekee. Akiwa "YANGA" alicheza kama Mshambuliaji na akiwa Taifa Stars alikuwa Golikipa "Tanzania One"!. Kwenye mechi baina ya Tanzania dhidi ya Kenya Desemba 9, 1967, KITWANA alikuwa kipa. Hadi mapumziko Kenya ilikuwa ikiongoza 3-0 huku Tanzania ikichezewa nusu uwanja. Kocha MILAN CELEBIC toka Yugoslavia akamhamishia KITWANA mbele. Mpira ulipoisha ubao wa magoli ulisomeka 3-3 ( KITWANA "Hat Trick" )!.
Kwa kutambua mchango wake wa kipekee wa soka nchini usio mfanowe, Juni 3, 2015, TFF ilimzawadia KITWANA Tuzo Maalum ukumbi wa JB Belmonte, Dsm katika kuadhimisha miaka 50 ya FIFA.
Aidha, Mei 26, 2017, TFF ilimzawadia KITWANA Tuzo ya Heshima ya Mchezaji Bora Kuliko Wote Nchini wa Zamani. Si YUNGE MWANANSALI wala MATHIAS KISSA aliyeweza kumpiku KITWANA!.
21. "YANGA" imetoa Mchezaji anaekubalika na wapenzi na wachezaji wenzake kuwa ndiye Bora kuliko wote waliowahi kutokea nchini ( SUNDAY MANARA "COMPUTER"). ABDALLAH KIBADENI (Mchezaji Bora wa Muda wote wa SIMBA) alikiri alipohojiwa na Azam Tv kuwa "Hakuna kama Sunday Manara ndio maana aliitwa Computer miaka ya 1970s wakati hata computers hazijaungia nchini "!. Aidha, KHALID ABEID, Kiungo Bora zaidi kuwahi kutokea SIMBA, alitanabaisha Agosti 23, 2020-: "Watu wanashangaa Benard Morrison anavyopanda mpira. Sunday Manara alikuwa anafanya hayo sana tena yeye alikuwa akisimama juu ya mpira na kupiga saluti huku mabeki wakishindwa kuuchukua mpira!".
22. "YANGA" imetoa mchezaji wa kwanza kucheza mpira wa kulipwa Ulaya ( SUNDAY MANARA ) aliyeenda kucheza Uholanzi 1976.
23. SIMBA imetoa mchezaji wa kwanza ( MBWANA SAMATTA ) kucheza Ligi Kuu ya Uingereza ambayo ndio Ligi pendwa na ngumu kuliko zote duniani .
24. "YANGA" imetoa mchezaji ( GIBSON SEMBULI ) aliyekuwa na mashuti makali kuliko wote waliowahi kutokea nchini. PETER TINO, FUMO FELICIAN & THUWEN ALLY wanasubiri kwa SEMBULI !!! SEMBULI alikuwa akiogopwa mno na makipa wa Ligi baada ya kuwa akichana nyavu mara kadhaa na pia alipomchana mkono MACHAPATI, kipa hodari wa Mwadui ya Shinyanga!.
25. "YANGA" imetoa mchezaji anaeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika msimu mmoja wa Ligi Kuu ( MOHAMED HUSSEIN "MMACHINGA"- 26 mwaka 1998 ).
26. "YANGA" Ilishinda "PAMBANO LA KIHISTORIA"
Watani wa jadi wamecheza mara 106 kwenye Ligi hadi leo lakini "Mtanange wa Kihistoria" ulipigwa uwanja wa Nyamagana, Mwanza Agosti 10, 1974. "YANGA" iliicharaza SIMBA mabao 2-1 kwa magoli ya GIBSON SEMBULI na SUNDAY MANARA.
27. SIMBA imetoa golikipa ( ATHUMAN MAMBOSASA) anaekubalika kuwa Kipa Bora kuliko wote waliowahi kucheza Ligi kwa mujibu wa mashabiki-wahenga na makipa mf IDD PAZI.
28. SIMBA imetoa kipa wa kwanza ( IDD PAZI "Father") kufunga kwenye mechi ya watani ambapo alifunga dakika ya 20, Machi 10, 1984.
29.SIMBA imetoa mchezaji ( MOSES ODHIAMBO ) anaeshikilia rekodi ya kufunga goli la mapema zaidi kwenye mechi ya Ligi baina ya watani ambapo alifunga dakika ya 2, Julai 8, 2007.
30. "YANGA" ni moja ya vilabu barani Afrika vyenye mataji mengi ya Ligi Kuu nchini mwao-:
1. Al Ahly- 41
2. Esperance Tunis- 29
3. "YANGA"- 27
4. El Hilal -27
5. ASEC Mimosa- 26
6. Asante kotoko- 24
31. Tamati
Hivyo basi, Utafiti huu mujarab umeonesha, pasina shaka, kuwa kihistoria "YANGA" ndio "Baba Lao" kwenye Ligi hapa nchini. Wapo watakaopinga utafiti huu kwa dhihaka. Hata hivyo, ni vyema wakarejea nukuu kuntu zifuatazo-:
1. "Utafiti haupingwi kwa matusi bali kwa Utafiti bora zaidi".
Kingunge Ngombale Mwiru, Juni 9, 2008.
2. "Facts are stubborn things; and whatever may be our wishes, our inclinations or the dictates of our passions, they cannot alter the state of facts and evidence".
Marehemu JOHN ADAMS, Rais wa Pili wa Marekani.
Na Mzee wa Atikali Atikaligbm@yahoo.com
0754 744 557
@Inalindwa na Haki Miliki

Tags:
michezo