ALIYEWAHI
kuwa Waziri wa Fedha wa Tanzania, Basil Pesambili Mramba amefariki
dunia leo Jumanne, Agosti 17, 2021 katika Hospitali ya Regency jijini
Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.
Mramba
aliwahi kuwa Waziri wa Fedha katika utawala wa Rais Jakaya Mrisho
Kikwete ambapo aliiongoza Wizara hiyo mwaka 2001-2005, baadaye Waziri wa
Viwanda, Biashara na Masoko mwaka 2006 hadi 2008.
Familia
ya Mramba imethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa ni
wanafamilia wachache wataruhusiwa kufika kutoa pole nyumbani kwa
marehemu, Mawenzi Road, Oysterbay jijini Dar.