SIMBA NA YANGA ZALETEANA BIFU UGENINI KENYA, CHANZO NI KUPANGWA HOTELI MOJA

Wakati ikiwa imesalia siku moja kuanza kurindima kwa michuano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya, miamba wa soka nchini Tanzania, Simba na Yanga wamegoma kulala Hotel Moja mjini Nakuru, Kenya.

Imeelezwa kuwa baada ya kuwasili nchini humo timu hizo mbili zilipangiwa kuweka kambi kwenye Hotel ya Midlands iliyopo mjini Nakuru lakini ziligoma kuwa pamoja eneo hilo.

Msala huo ulitokea mpaka ambapo ikabidi watenganishe na Yanga walisalia kwenye Hotel hiyo huku Simba ikabidi wapelekwe sehemu nyinginr tofauti na hiyo ambayo watani zao wa jadi waliamua kusalia.

Michuano hiyo inayoanza kesho Jumapili, itaanza kwa Yanga kukipiga na Kakamega Home Boys kuanzia majira ya saa 7 kamili mchana huku JKU ya Zanzibar ikicheza na Gor Mahia FC saa 9 mchana.

Wakati huo Simba yenyewe itaanza kibarua chake Jumatatu ya wiki ijayo Juni 4 2018 kwa kukipiga na Kariobang Charks kuanzia majira ya saa 9 kamili mchana.

Post a Comment

Previous Post Next Post