BARUA YA KKKT YAMSIMAMISHA KAZI MSAJILI MAMBO YA NDANI

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amemsimamisha kazi msajili wa vyama wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Merlin Komba kuhusiana na sakata la barua waliyoandikiwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, (KKKT) na wizara hiyo wakitakiwa kuufuta waraka wa pasaka ndani ya siku kumi.

Komba ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii.

Akizungumza na wanahabari leo, Juni 8, Dk Mwigulu amesema Serikali ikiwabaini waliotengeneza barua watawachukulia hatua kwani imesababisha taharuki.

Dk Mwigulu amesema kabla hata ya Serikali kutoa kauli, wamejitokeza watu waliotoa msimamo wakiwamo wenye vyama vya siasa.

“Kwani kuna faida gani tukipoteza amani ya nchi yetu?” Amehoji Dk Mwigulu.

MWANANCHI

Post a Comment

Previous Post Next Post