Yanga hivi sasa ipo kwenye mipango ya kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao na kati ya safu ambayo inahitaji marekebisho ni safu ya ushambuliaji inayoandamwa na wachezaji wengi majeruhi nao Amissi Tambwe na Donald Ngoma ambaye tayari ameshachukuliwa na Azam.
Walcott alikuwepo kwenye kikosi cha APR kilichotolewa na Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2016 kwa kufungwa mabao 2-1 na yeye alikuwa tishio kwenye safu ya ulinzi ya Wanajangwani.
Akizungumza nasi kutoka Rwanda, Walcott alisema yeye mkataba wake unamalizika Julai 3, mwaka huu hivyo yupo tayari kujiunga na Yanga kama wana nia ya kumsajili kwa ajili ya msimu ujao.
Aliongeza kuwa, wapo wachezaji waliomvutia yeye kuja kucheza soka nchini hapa akiwemo kiungo mchezeshaji Mnyarwanda. Haruna Niyonzima anayeichezea Simba akitokea Yanga baada ya mkataba wake kumalizika msimu uliopita.
“Ni muda wangu muafaka umefika wa mimi kuondoka hapa Rwanda na kuja kucheza soka la kulipwa Tanzania na nipo tayari kujiunga na timu itakayovutiwa na mimi ikiwemo Yanga ambayo nimepata taarifa za kuhitaji mshambuliaji.
“Pia, nipo tayari kuzichezea timu nyingine kama Simba, Singida na nyingine zozote kikubwa nitaangalia maslahi pekee yatakayonishawishi mimi kusaini.
“Mimi hadi hivi sasa nimefunga mabao saba na anayeongoza ana mabao 11 wakati ligi ikielekea ukingoni,” alisema Walcott anayetumia miguu yote miwili katika kupiga mashuti.
Alipotafutwa Niyonzima kumzungumzia mshambuliaji huyo alisema “Jamaa anajua. Ni mchezaji mzuri na ni kati ya washambuliaji wanaokuja
Tags:
michezo