
Baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara, mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi amewashukuru mashabiki wa Simba na kuahidi kutoa zawadi kwa mashabiki wawili.
Kupitia ukurasa wake wa instagram @emmanuelokwi ametoa ujumbe huo kwenda kwa mashabiki.
“Mmekuwa zaidi ya mashabiki msimu huu, mmenipa thamani kubwa. Niliporudi mlinipokea kwa mikono miwili hiyo ilinipa nguvu ya kuwapambania kila tuingiapo uwanjani.”
“Kesho nataka kutoa zawadi ya kipekee kwa mashabiki wawili kama shukrani kwa upendo wenu. Nawapenda sana.”
Okwi anatarajia kutwaa tuzo ya ufungaji bora msimu huu akiwa na magoli 20 hadi sasa ukiwa umebaki mchezo mmoja huku akifuatiwa na John Bocco ambaye ana magoli 14 katika msimamo wa wafungaji bora 2017/18.
Tags:
michezo