Warembo wawili ambao walifahamika kwa majina ya Ashura na Zubeda, wamedaiwa kuzichapa kavukavu chanzo kikitajwa kuwa ni kumgombea baba wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma.
Tukio hilo lililokusanya watu lilitokea hivi karibuni katika baa moja maarufu kwa jina la Suma iliyopo maeneo ya Magomeni-Kagera jijini Dar ambayo baba wa msanii huyo anadaiwa kuwa anakwenda mara kwa mara kupata ‘kinywaji’.
Taarifa zaidi zinaarifu kuwa, warembo hao walitangulia kufika katika baa hiyo na kupiga stori pamoja huku wakipata kilevi lakini baadaye alipotokea baba Diamond na kujumuika nao, kila mmoja alianza kujitapa kuwa ni wake.
“Yani walianza kubishana. Ghafla wakaanza kushikana na ndipo watu walipowawahi na kuwaamua. Baba Diamond kukwepa soo akaamua kutoweka eneo hilo,” kilidai chanzo