BAADA YA YANGA KUPOKEA KICHAPO KUTOKA KWA AZAM, MASHABIKI WAUCHARUKIA UONGOZI WA KLABU HIYO

Mashabiki wa klabu ya Yanga wametoa malalamiko yao juu ya mwenenndo mzima wa timu yao.

Haya yamekuja baada ya yanga kumaliza vibaya msimu wa ligi kuu Tanzania bara kwa kupokea kichapo cha goli 3-1 dhidi ya Azam FC mechi iliyochezwa uwanja wa Taifa.

Baada ya mechi hiyo mashabiki waliutupia lawama uongozi wa klabu kwa kushindwa kuweka mambo sawa ili timu iweze kufanya vizuri.

Pia mashabiki hao wameutaka uongozi wa klabu hiyo kujipanga na kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri msimu ujao.

Post a Comment

Previous Post Next Post