
Bodi ya ligi imetoa taarifa ya marekebisho ya mchezo mmoja namba 199 kati ya Mbeya City na Yanga uliokuwa umepangwa kufanyika Mei 1-2018 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya, sasa utapangiwa tarehe nyingine.
Kulingana na taarifa hiyo, uamuzi wa kuipangia tarehe nyingine ni kukidhi matakwa ya Kanuni inayotaka nafasi kati ya mechi moja na nyingine isiwe chini ya angalau saa 72.
Yanga itacheza na Simba Aprili 29-2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivyo isingekuwa rahisi kucheza May Mosi, ikiwa ni siku mbili tu zinazokuwa zimepita.
Tags:
michezo