
Mfaransa huyo alisema amewasisitiza wachezaji wake wasibweteke kwa mafanikio waliyonayo sasa ikiwamo kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara na kusonga mbele kwenye michuano ya Afrika, akisema kibarua kipevu kipo mbele yao.
Kocha Lechantre amewatamkia wachezaji wake kuwa wanatakiwa kupambana kila siku ili kufikia lengo na kutengeneza historia katika Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho.
“Nipo Simba, zaidi ya mwezi sasa naona kila mchezaji anajitahidi kujitolea kwa nafasi yake, ila kwa kweli bado kazi wanayo, tunataka tuwe miongoni mwa timu zitakazocheza makundi Afrika, ndio maana nawataka wasilale kabisa,” alisema.
“Tunakabiliwa na mechi ngumu na muhimu katika mashindano tunayoshiriki, hivyo kila mmoja lazima ajipange na kupambana ili tufanye vizuri na kuweka rekodi.”
Simba itaikaribisha Al Masry ya Misri Machi 6 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kabla ya kuwafuata ugenini siku 10 baadaye kwa mchezo wa marudiano ili kuamua ya kusonga mbele kucheza play-off katika kwa lengo la kufuzu makundi.
Timu hizi zilipenya katika mechi zao za awali kwa Simba kuing’oa Gendarmarie ya Djibouti kwa mabao 5-0, huku Wamisri wakiwatoa nishai Green Buffaloes ya Zambia kwa mabao 5-2, ikishinda nyumbani kwao mabao 4-0 na kulala ugenini mabao 2-1
Tags:
michezo