
Emmanuel Okwi alitolewa nje ya uwanja dakika ya 76 ya mchezo baada ya kuumia, na nafasi yake kuchukuliwa na Mrundi Laudit Mavugo,
Simba wametoa taarifa kupitia kwenye ukurasa wao wa Instagram kuwa Okwi anaendelea vizuri kutoka kwenye majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mbao FC.
Daktari wa Simba Ndg: Yassin Gembe amesema kuwa hali ya Okwi ni nzuri, 'Okwi anaendelea vizuri sana tofauti na jana, kwa hali aliyonayo pamoja na tiba ambazo tumeshampatia ni asilimia kubwa sana kwa yeye kuwepo kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Stand United Ijumaa hii'
Mchezo unaofuta katika raundi ya 20 Simba wataikaribisha Stand United (chama la wana) kutoka mkoani Shinyanga Ijumaa ya March 02-2018 kwenye uwanja wa Uhuru/Taifa-Jijini Dar es salaam saa 16:00 jioni.
Katika chati ya msimamo Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 45 katika michezo 19 ikifatiwa na Yanga ambao wana alama 37, huku wakiwa na mechi 18, Azam Fc wao wako nafasi ya 3 wakiwa na alama 35 kwa michezo 19.
Tags:
michezo