
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba amesema gharama ya hati ya kusafiria mpya ya kielektroniki itakuwa Sh150,000.
Dk Nchemba amesema hayo leo Jumatano Januari 31,2018 wakati wa uzinduzi wa hati ya kusafiria ya kielektroniki jijini Dar es Salaam.
Amesema kiasi hicho ni sawa na Sh15,000 kwa mwaka kwa sababu itatumika kwa miaka 10.
Gharama za kupata pasipoti sasa ni Sh50,000 na hutumika kwa miaka 10 tangu zilipotolewa.
Dk Nchemba amesema pasipoti hizo zitakuwa na kurasa nyingi zaidi na mwonekano mpya.
Kamishna wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala amesema kuanzia sasa mtu atakayetaka hati ya kusafiria atapaswa kuwa na kitambulisho cha Taifa.
Amesema hati za sasa zitaendelea kutumika hadi Januari 2020.
MWANANCHI
Tags:
habari