
Mwenyekiti wa usajili Klabu ya Yanga Hussein Nyika amefunguka kuwa
” Ngoma alikuwa mgonjwa mwalimu wake kamuona ameshapona ameamua kumuita, Hawawezi kusema ni mchezaji huru wakati ni mchezaji wa Yanga na Anamkataba nafikiri ni makosa ya Kiuandishi ”
Nyika amesema aliongea na Ngoma siku kadhaa zilizopita na Ngoma akamwambia amepona na mwishoni mwa wiki hii angetua Yanga lakini bila kabla ya hayo kutimia ameitwa timu ya Taifa.
Nyika amesema pia Ngoma alipoumia Yanga walitaka kwenda kumtibu Afrika Kusini lakini mwenyewe alikataa na kusema kuwa ataenda kutibiwa kwa daktari wake Aliyepo Zimbabwe ambapo ni kwao kabla ya Baadhi ya Viongozi kudai kuwa aliondoka bila kuaga.
Tags:
michezo