SIMBA YASAJILI BEKI WA HATARI KUTOKA GHANA

Klabu ya Simba inasadikika kuwa beki Mghana, Malik Ismaila anae kipiga katika klabu ya Tema Youth ambaye pia anakipiga katika timu ya taifa ya chini ya miaka 23.

Beki huyo alitua siku ya Jumamosi kwa ajili ya mazungumzo na Wekundu hao jambo linaloashiria kuna staa mmoja wa kigeni atakatwa.

Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema mchezaji huyo mwenye kimo kama cha Juuko Murshid, ana nafasi kubwa ya kusajiliwa kwenye dirisha dogo kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo anayekwenda Gor Mahia ya Kenya kwa mkopo.

Ujio wa mchezaji huyo aliyefikia hotelini Kariakoo, unamaanisha Joseph Omog lazima afanye maamuzi magumu kama bado ana msimamo wa kumsajili straika wa Rayon ya Rwanda, Shazir Nahimana.
LIKE. 







Post a Comment

Previous Post Next Post