KOCHA WA AZAM SC AVURUGWA NA ADHABU YA TFF


Kocha wa Azam, Aristica Cioaba haelewi kwanini amepewa adhabu ya kukosa mechi tatu kukaa katika benchi lakini akizungumzia usajili wa straika wake mpya Bernard Arthur kuwa ni mtu anayemjua vyema.

Mromania huyo alisema alikuwa anataka kusajili mshambuliaji mwenye kasi na ujuzi wa kufunga vitu ambavyo Arthur anavyo ambapo vitaongeza kitu tofauti katika safu yake ya ushambuliaji.

Alisema Ligi ya Tanzania inahitaji kuwa na mshambuliaji aina ya Arthur ambapo endapo ataelewana vyema na Mbaraka Yusuf wataleta matokeo mazuri kwa Azam.

"Sijasajili mtu ambaye simjui namjua vyema Arthur ni mshambuliaji niliyekuwa namtaka anajua kufunga na kasi ambayo itamsaidia kucheza hapa Tanzania,"alisema Cioaba.

"Ligi inahitaji mshambuliaji aina ya Arthur na ndiyo maana nimesajili kama akiwahi kuelewana na wenzake tutakuwa tumeongeza kitu kikubwa katika safu yetu ya ushambuliaji."

Post a Comment

Previous Post Next Post