HAYA HAPA MATOKEO YA AZAM FC vs MTIBWA SUGAR

Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea jana kwa mchezo mmoja uliokuwa unakamilisha raundi ya 11 ya VPL 2017-2018.

Katika kukamilisha raundi hiyo Azam Fc waliikaribisha Mtibwa Sugar katika Uwanja wao wa nyumbani Azam Complex (Chamanzi).

Mchezo huo ulianza majira ya saa 19:00 za usiku huku timu zote zikihitaji pointi 3 muhimu ili kujiweka sawa katika mbio za Kuwania ubingwa wa ligi.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinaisha timu hizo zililazimishana sare ya kufungana goli 1-1, goli la Azam Fc lilifungw na Enock Atta Agyei katika dakika ya 57 ya mchezo.

Goli la kusawazisha la Mtibwa Sugar na Kelvin Kongwe Sabato kwa 'free-kick' kunako dakika ya 75 ya mchezo.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa hivi: Razack Abarola, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Yakubu Mohamed, Agrey Moris, Salmin Hoza, Salum Abubakar, Frank Domayo, Mbaraka Yusuph, Yahya Zayd, Enock Atta.

Kikosi cha Akiba kilikuwa hivi.
Mwadini Ally, David Mwantika, Masoud Abdallah, Ramadhan Singano, Paul Peter, Stephen Kingue, Idd Kipagwile

Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa hivi:
Benedict Tinoco, Rogers Gabriel, Issa Rashid, Dickson Daud, Kassian Ponera, Shaaban Nditi, Ally Makarani, Mohamed Issa, Stamil Mbonde, Hassan Dilunga, Salum Kihimbwa.

Kikosi cha Akiba kilikuwa hivi.
Abubakar Msheri, Hassan Idd, Salehe Hamisi, Hassan Mganga, Rifat Khamis, Haruna Chanongo, Kelvin Kongwe.

Baada ya kukamilika kwa mechi zote za raundi ya 11, msimamo wa ligi unaonesha Simba bado kileleni, huku klabu ya Stand United ikiwa nafasi ya mwisho

Post a Comment

Previous Post Next Post