
Benchi la Ufundi la Klabu ya Yanga Kupitia kwa Kocha wake Mkuu George Lwandamina limesema Halina wasiwasi juu ya Pengo la Papy Kabamba Tshishimbi kuelekea Mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.
Yanga itakosa Huduma ya kiungo huyo mkabaji ambaye atakuwa akitumikia adhabu ya kutocheza mchezo mmoja mara baada ya kupata kadi tatu za njano Tshishimbi amecheza kwa asilimia mia(Michezo Yote dakika zote) katika michezo minne ya Mwanzo.
Kesi ya Manji Kuendelea Leo.
Kesi ya utumiaji wa madawa ya kulevya ya aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji inatarajiwa Kuunguruma leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Manji leo anatarajiwa kupeleka Mashahidi kwaajili ya Kutoa utetezi wao,Kesi hiyo inatarajiwa Kuendelea Kusikilizwa leo na Kesho.
Tambwe Leo anarejea Mazoezini
Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Amisi Joslyn Tambwe leo jumatatu anatarajiwa kurejea katika mazoezi kufuatia kukaa benchi toka Ligi Imeanza, Tambwe alikuwa na maumivu ya Goti, Daktari wa Timu ya Yanga Dr. Bavu amethibitisha kuwa Tambwe yuko fiti kwa Sasa na leo ataanza mazoezi Mepesi. Like Ukurasa wetu wa Facebook hapo chini ili kuzipata kali za Kimichezo kila siku
Tags:
michezo