
Mtumishi wa Mungu na mwimbaji wa nyimbo za injili Moses Malele kutoka Arusha mjini, amekusogezea albamu yake mpya inayokwenda kwa jina la TUTAVUKA...
Kama utakumbuka mwimbaji huyu amekuwa baraka sana katika kuifanya kazi ya Mungu kwa njia ya uimbaji wa nyimbo za injili kwa muda mrefu kupitia kwaya mbalimbali akiwa kama mwimbaji na wakati akitumika kama mwalimu wa nyimbo kwenye kwaya hizo.
Baadhi ya kwaya ambazo ametumika ni pamoja na kwaya ya Malampaka iliyojulikana kwa albam za GEUKA na SIMAMA NA MWOKOZI, Emmaus Band iliyotamba na Albam ya VITA NA SHETANI pia kwaya ya MWADUI...
Moses Malele kwa sasa yupo mjini Arusha akitumika shambani mwa Bwana kwa njia ya uimbaji, kuhubiri na mwalimu wa semina mbalimbali (+255758304211), hivyo amekuletea albam yake mpya ya TUTAVUKA
BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA KAZI YAKE>>>