ARSENAL, CHELSEA ZAKUBALIANA KUHUSIANA NA UHAMISHO WA OXLADE-CHAMBERLAIN

Chelsea na Arsenal zimekubaliana kuhusiana na uhamisho wa Alex Oxlade-Chamberlain.

Chelsea imekubali kutoa pauni milioni 35 kumnasa na mambo yakienda vizuri, huenda leo akafanya vipimo.

Katika mechi iliyopita, Arsenal ilitwangwa mabao 4-0 na Liverpool huku Oxlade-Chamberlain akicheza kama beki wa kulia, jambo lililozua mjadala mkubwa kuhusiana na uamuzi huo wa Kocha Arsene Wenger kumpanga katika nafasi hiyo.

Siku chache zilizopita, Oxlade-Chamberlain alikataa kuongeza mkataba na Arsenal na mshahara wake ungekuwa pauni 180,000 kwa wiki!
Previous Post Next Post