BEYONCE NA JAY-Z WAMPA JINA LA KIISLAM MTOTO WAO

Baada ya kujifungua mapacha wiki kadhaa zilizopita sasa,Beyonce na mume wake Jay-Z wabainisha majina ya wanao wawili .

Mapacha wa magwiji wa sanaa ya Muziki kutoka Marekani wamepewa majina ya Rumi na Sir .

Rumi ni jina la mwanafalsafa wa kiislamu aliyeishi katika karne ya 13 ambaye hadi wa leo anakumbukwa kwa kazi yake ya mashairi na maneno yaliyopendekeza upendo ,furaha na uvumilivu .

Wasanii hao nyota wamesemekana kuwakilisha haki ya miliki kwa majina ya wanao kama Rumi Carter na Sir Carter ili kuhakikisha kwamba hamna mtu mwengine atakayefaidi kutokana na majina hayo .
Previous Post Next Post