ALICHOPOSTI MTATIRO BAADA YA TAMKO LA RAIS MAGUFULI

Kupitia Ukurasa wake wa Facebook Mtatiro ameandika hivi...

"SERIKALI.....

SERIKALI I
"Serikali imeweka dira itakayowawezesha wasichana kuendelea na masomo baada ya kujifungua huku wale waliowapa mimba, wakishughulikiwa kikamilifu." Paulina Mkonongo, Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari, Wizara ya Elimu - 01 Disemba 2015.
______________________________________________
SERIKALI II
"Serikali imeamua kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni wasifukuzwe, bali waendelee na masomo." Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, akiwa Chuo kikuu kishiriki cha UDSM cha Elimu (DUCE), 27 Aprili 2017.
______________________________________________
SERIKALI III
"Serikali inaelekeza Wasichana wanaojifungua warudi na kuendelea na masomo shuleni." Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (06 June 2017- Gazeti la The Citzen).
______________________________________________
SERIKALI IV
"Katika kipindi changu cha utawala, mwanafunzi yeyote wa kike (shule ya msingi na sekondari) akipata mimba ni marufuku kurudi shuleni. Siwezi fanya kazi ya kusomesha wazazi." Rais John Pombe Magufuli, 22 Juni 2017, Bagamoyo - Pwani.
______________________________________________
#MASWALI;
1. Hivi Serikali ni mtu mmoja au ni muunganiko wa watu wengi?
2. Sera za Serikali zinapitishwa na mtu mmoja mmoja au na vyombo?
3. Tanzania inajenga TAASISI imara? Au WATU imara?
#JSM.
Previous Post Next Post