Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi askari 12 waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya wakati uchunguzi ukiendelea.
“Tumeamua kuwasimamisha kazi wote walioguswa moja kwa moja na sakata hili, pia Polisi itachukua hatua madhubuti ikiwemo kuwapeleka mahakamani wasanii waliotuhumiwa,” alisema.
Askari hao ni wale waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda siku mbili zilizopita wakati akiwaambia wanahabari juu ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara na matumizi ya madawa hayo.
Tags:
habari