ISHU YA MAYELE KUONDOKA AU KUBAKIA YANGA IKO HIVI
Licha ya kufanya siri kubwa, lakini soka la bongo imevidaka za chini ya kapeti kuwa vigogo wa Yanga juzi usiku walikuwa na kikao kizito na Fiston Mayele nyumbani kwake Mbezi Beach karibu na ufukwe wa Bahari ya Hindi
Kikao hicho kilihusisha pia wasimamizi wa mchezaji huyo ambao wanapushi staa huyo akakiwashe Arabuni ambako kuna mkwanja mnene na wako tayari kununua mkataba uliosalia Yanga.
Bado hawajafikia muafaka wa kusalia au kuondoka ingawa tajiri kaahidi dau nono lakini jana mchana pia Mayele alionekana sehemu akipiga picha za matangazo ya uzi mpya wa Yanga jambo ambalo linaashiria lolote linaweza kutokea na akaonekana ameshikilia uzi mpya wa Jangwani.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: