
Msemaji wa zamani wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema timu inapaswa kwenda Nigeria kwa tahadhari zote kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ugenini.
Manara amesema viongozi, benchi la ufundi, wachezaji, mashabiki na wanachama hawapaswi kuweka vichwani mwao matokeo ya mchezo dhidi ya Simba kwani umeshapita
Amwswma Yanga inapaswa kujipanga vyema kuhakikisha wanaweza kupata ushindi dhidi ya Rivers United na kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika
"Tuna mechi muhimu sana Nigeria, tunapaswa tuweke nguvu zetu huku ili kuhakikisha tunakwenda kufanya vizuri ugenini na kuja kumaliza kazi nyumbani"
"Hatuna sababu ya kuendelea kufikiri matokeo ya mchezo uliopita shidi ya Simba, zaidi tutumie kama funzo kuelekea mchezo unaofuata, hatupaswi kuwadharau wapinzani wetu"
"Huu ni wakati wa kazi sasa, tuache maneno mengi kabla ya mechi, twende tukaipiganie nembo ya Yanga na kuweka historia kubwa katika soka la Tanzania" alisema Manara
Yanga inakabiriwa na mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali kombe la shirikisho baeani Afrika dhidi ya Rivers United ambao utapigwa Jumapili April 23 huko Nigeria
Yanga itakwenda Nigeria ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza dhidi ya Rivers United mwaka 2021 katika michuano ya ligi ya mabingwa
Mechi mondo wa pili itakamilishwa jijini Dar es salaam katika uwanja wa Benjamini Mkapa April 30.
0 Comments