FAMILIA YAUGUA UGONJWA WA AJABU HUKO BABATI

Helena Hungoli

Familia moja huko katika Wilaya ya Babati mkoani Manyara iliyopo katika kijiji cha Imbilili Juu, imekumbwa na ugonjwa wa ajabu baada ya watu wa familia hiyo ambao ni Helena Hungoli mwenye umri wa miaka 60 anayeishi na ndugu zake wengine kukumbwa na ugonjwa wa ajabu wa ngozi kuning’inia na kufunika pua na mdomo.

Pia katika familia hiyo wapo watoto wawili ambao ni watoto wake na Helena Hungoli, pamoja na ndugu zake ambao wote wanaishi kwenye kibanda kidogo wameugua ugonjwa huo.

Helena ameiomba Serikali na wasamaria wema kumsaidia, kwa kumuwezesha kutibu tatizo la ugonjwa huo ambao amedumu nao kwa zaidi ya miaka 55.

Wakati akizungumza amesema kwa sauti ya chini yenye majonzi:

“kila sehemu ya mwili wangu inauma na kwa hali niliyo nayo, inanibidi nishinde nyumbani muda wote na sasa nahitaji msaada mkubwa, Serikali na wasamaria wema nisaidieni”

Kwa sasa amesema hawezi kufanya kazi yoyote ya kumuingizia kipato, kutokana na kuwa na hali ya ugonjwa huo tangu akiwa mdogo hadi sasa, hivyo ameiomba Serikali na wasamaria wema kuweza kumsaidia yeye pamoja na familia yake kuondokana na tatizo la ugonjwa huo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.