KUMEKUCHA!! SIMBA NA YANGA KUKUTANA LEO JUMAMOSI, KOCHA WA YANGA AWATISHIA SIMBA
KOCHA Mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema ‘Morinyo’ ameweka wazi kuwa anataka kufuta uteja mbele ya Simba Queens kwa kushinda kwenye mechi yao ya dabi itakayopigwa leo Jumamosi katika Uwanja wa Mkapa, Dar.
Kocha huyo alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano kati ya timu hizo na Waandishi wa Habari uliofanyika jana Ijumaa katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Edna alisema: “Sina matokeo mazuri au Yanga Princess haina matokeo mazuri mbele ya Simba, ila huu ni mchezo na matokeo ni baada ya dakika 90, tumejiandaa kushindana na kushinda.”
Kwa upande wake nahodha wa Yanga Princess, Fatuma Mwisendi, alisema: “Tutahakikisha tunapambana, tutaonyesha mchezo mzuri na wa kiungwana ukizingatia kuwakikosi chetu kina wachezaji wazoefu, wengi wao wameshacheza dabi tofautinchini kwao, kwa hiyo sidhani kama mchezo wa kesho (leo) utatuzuia sisi kupata ushindi.”
Nahodha wa Simba, Violeth Nicholas, alisema:“Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo huu, muhimu ni kuboresha muendelezomzuri tulionao kwenye ligi na kushinda mechi zetu na kubakia nafasi ya kwanza kwenyemsimamo.”
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: