juu ya kurejea wa kiungo wa zamani wa Simba, Clatous Chama raia wa Zambia, uongozi wa klabu hiyo ukiongozwa na Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez wamefanya kikao na wazazi wa mchezaji huyo baada ya mchezo wao wa marudiano na Red Arrows uliofanyika jijini Lusaka, juzi.Barbara alisisitiza jana kwamba; “Dirisha dogo linakwenda kufunguliwa tunasubiri ripoti ya Kocha. Lakini kwa aina ya mchezo tuliouona na malengo yetu lazima tufanye maamuzi magumu sasa kwa kusajili wachezaji wazuri zaidi, ili tupate mafanikio tunayoyataka kwenye michuano hii ya Afrika.”
Simba ilimuuza Chama katika timu Berkane RBS ya Morocco lakini imeonyesha kuwa hana wakati mzuri kwenye kikosi hicho hivyo ameonyesha nia ya kutaka kuachana nao lakini klabu hizo kongwe hapa nchini Simba na Yanga kila moja imekuwa ikitajwa kutaka kumnasa nyota huyo.
Hata hivyo, upepo ni mzuri kwa Simba ambao walimuuza nyota huyo huku ikidaiwa kuwa katika makubaliano yao ya mkataba na Berkane walikubaliana kwamba endapo mchezaji huyo watataka kumuuza ama kumtoa kwa mkopo basi kipaumbele iwe timu yake hiyo ya zamani.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba,Mulamu Ng’hambi aliliambia Mwanaspoti jana akiwa Zambia kuwa, ujio wa wazazi wa Chama, baba na mama yake ni kuwasalimia wachezaji na viongozi ambao walikuwa wakiishi na mtoto wao vizuri.
Licha ya kugoma kufafanua kama wameshaanza mazungumzo siriazi ya kumrejesha mchezaji huyo kundini lakini alisisitiza kwamba; “Kama Chama atarudi Tanzania atakuja kucheza Simba, hawezi kwenda Yanga wala klabu nyingine nisikilize mimi.” Pamoja na kauli hiyo, lakini Mwanaspoti linajua kwamba Yanga nao wako kwenye mazungumzo na vigogo wa Berkane na wakala wa Chama kuhakikisha wanamnasa mchezaji huyo. Chama kwenye mahojiano yake maalum na Mwanaspoti wiki iliyopita alisisitiza kwamba; “Nimesikia mambo mengi kwenye mitandao lakini muda utaongea. Nikisema nizungumze kiundani zaidi yanaweza kutafsiriwa tofauti.”
0 Comments