ALICHOSEMA CHAMA BAADA YA TETESI ZA KUVUNJA MKATABA RS BERKANE

Mara baada ya kuwepo kwa tetesi juu ya mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba SC Clouts Chama ambaye anachezea klabu ya RS BERKANE ya Morocco kuwa amevunja mkataba na klabu yake, mchezaji huyo amekanusha taarifa hizo. Chama amesema taarifa hizo si za kweli kwani yeye bado ni mchezaji halali wa timu ya RS BERKANE.

''Sijui kwanini watu wanaandika stori kubwa za uongo kama hizo, hakuna ukweli kuhusu hilo, mimi bado ni mchezaji halali wa RS BERKANE'' alisema Chama

Post a Comment

0 Comments