HII HAPA IDADI YA MIILI YA WATU ILIYOPATIKANA KATIKA ZIWA TANGANYIKA BAADA YA AJALI YA BOTI
Hadi sasa jumla ya miili 13 imepatikana katika Ziwa Tanganyika baada ya boti mbili kugongana eneo la Rubengera wilayani Uvinza hapo juzi na watu 22 kuhofiwa kufariki.
Miongoni mwa waliokuwa katika boti hizo, ni waumini wa Makanisa ya PEFA waliokuwa wakielekea kwenye mkutano wa injili eneo la Sunuka.
-
Afisa mfawidhi wa SUMATRA mkoani Kigoma amesema kupatikana kwa miili hiyo ni baada ya kuwatumia waokoaji wa majini na zoezi la kutafuta miili zaidi linaendelea.
Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
No comments: