ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA JOSEPH OMOG AELEZA PRESHA KUBWA ALIYOKUWA AKIIPATA NDANI YA SIMBA

Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon amefunguka kuwa kabla ya mabosi wa timu hiyo kumtimua, alikuwa na presha kutokana na mwenendo wa timu hiyo ulivyokuwa.


Maisha ya kocha huyo Simba yalifikia tamati juzi Jumamosi baada ya mabosi wa timu hiyo kuamua kumtimua kutokana na matokeo mabaya ya klabu hiyo, hasa baada ya kutolewa kwenye Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Green Warriors iliyo Daraja La Pili (SDL).

Simba ambao ni mabingwa wa kombe hilo, walitolewa kwa penalti 3-4 dhidi ya Green Warriors katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar, Ijumaa iliyopita.

Omog ambaye aliwahi kuifundisha Azam amesema kuwa alikuwa na presha kubwa katika klabu hiyo katika kila mchezo wao ikiwemo dhidi ya Green Warriors ambao ndio ulitamatisha maisha yake ndani ya klabu hiyo iliyo kileleni mwa ligi na pointi 23.

“Kila siku kwangu ndani ya Simba nilikuwa nina presha hasa kwenye mechi zetu bila ya kujali kwamba tulikuwa tunashinda, tunafungwa au sare, kikubwa kwangu ilikuwa ni presha kwani matokeo ya timu yalikuwa yanatazamwa na watu wengi, jambo ambalo lilikuwa linanipa hofu,” alisema Mcameroon huyo.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa

No comments:

Powered by Blogger.