KOCHA WA SIMBA AMTAJA MCHEZAJI WA YANGA ALIYEHARIBU MIPANGO YAO YA USHINDI DHIDI YA YANGA

Baada ya sare ya goli 1-1 pambano ka watani wa Jadi, juzi Jumamosi kocha Mkuu wa Sinba Sc, Joseph Omog amefunguka na kutaja kiungo aliyeharibu mipango yao ya Ushindi.

Kocha huyo alimtaja Papy Kabamba " Tshishimbi kuwa alicheza vema kwenye nafasi yake na kwamba yeye alikuwa kikwazo kikubwa kilichosababisha timu yake kutoa sare.

Tshishimbi alitua Yanga akitokea Mbabane ya Swaziland na huu ni mchezo wake wa pili kucheza na Simba baada ya kucheza nao ule wa Ngao ya Jamii.

"Ni mchezaji mzuri sana, anaijua kazi yake vizuri. Alikuwa kikwazo kikubwa sana kwetu," alisema Omog alipokuwa akimuekezea Tshishimbi.

Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 753 336 000 au +255 625 917 902

Masengwa blog Ipo Play Store…Download HAPA ,Uwe unapata habari zote kwa urahisi zaidi
 Bofya Hapa
Powered by Blogger.